27 Agosti 2025 - 09:48
Matokeo Chanya ya Ziara ya JMAT-TAIFA Katika Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Kuhusu Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA)

Kwa kutambua mchango huo, JMAT-TAIFA iliishukuru na inaendelea kuishukuru kwa dhati Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ushirikiano wao madhubuti, na walisisitiza kuwa mshikamano huo utaendelea kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii zote za Taifa pendwa la Tanzania

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) -ABNA- Moja ya ziara muhimu za maendeleo na ustawi wa jamii zilizofanywa na zinazofanywa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA), ambayo itabaki daima katika kumbukumbu za JMAT, ilifanyika hivi karibuni kupitia ziara ya Mwenyekiti wa JMAT-TAIFA, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Matokeo Chanya ya Ziara ya JMAT-TAIFA Katika Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Kuhusu Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA)

Katika ziara hiyo, Sheikh Dkt. Alhad Mussa Salum aliambatana na Mratibu wa JMAT-TAIFA, Ukhti Fatma Frederick Kikkides, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mipango, Fedha, Uchumi na Utekelezaji (IMFU) JMAT-TAIFA, Ndugu Ayoub Joseph Sanga.

Viongozi hawa wa JMAT-TAIFA walitumia fursa ya mazungumzo na viongozi wa Wizara kuwasilisha mpango wa kushirikiana katika maandalizi ya Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA).

Kwa upande wake, Wizara iliahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kufanikisha tukio hilo, huku ikitoa muongozo na ushauri wa kina juu ya namna bora ya kufanikisha zoezi hilo la kijamii na kitaifa.

Aidha, Wizara iliunganisha JMAT na vyombo vya habari hususan AZAM TV, sambamba na kuipatia jumuiya hiyo wataalamu wa kushirikiana nao katika utekelezaji wa shughuli husika. Pia viongozi wa Wizara waliahidi kuendeleza ushirikiano wa karibu na JMAT kwa ajili ya kufanikisha Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA) na shughuli nyingine zenye maslahi mapana kwa taifa.

Kwa kutambua mchango huo, JMAT-TAIFA iliishukuru na inaendelea kuishukuru kwa dhati Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa ushirikiano wao madhubuti, na walisisitiza kuwa mshikamano huo utaendelea kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa jamii zote za Taifa pendwa la Tanzania.

Matokeo Chanya ya Ziara ya JMAT-TAIFA Katika Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo Kuhusu Matembezi ya Hiari ya Amani (MHA)

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha